Header Ads

TANZANIA YA VIWANDA YAANZIA INYALA MBEYA




          Mbeya.  Wakulima 3,000  mkoani hapa wataingia mkataba na Kiwanda kipya
cha  kusindika pareto kiitwacho Tan Extracts kilichopo katika Kijiji
cha Inyala  ili wazalishe pareto bora na kuuza zao hilo kwa bei kubwa
kwenye kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mtendaji  wa kiwanda hicho, Zavedi Chelele alisema hayo
mwishoni mwa wiki wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi uliofanywa na
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Amour Hamad Amour ukiwa katika
Halmashauri ya Mbeya
.
Chelele alisema ujenzi wa kiwanda hicho ulianza mwaka jana na  kwa
sasa umekamilika kwa asilimia 90 na kwamba tayari wakulima 1,000
wameingia mkataba  na kiwanda hicho huku lengo likiwa ni kuwafikia
wakulima 3,000
.



Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho Martin Oweka , alisema zaidi
ya Sh530 milioni zimetumika kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda hicho
mkoani hapa na kwamba kitakuwa cha pili hapa nchini baada ya kiwanda
cha pareto Mafinga mkoani Iringa.
Oweka alisema  kiwanda kwa sasa kimeajiri watumishi 11 na kwamba baada
ya kukamilika watakuwa wafanyakazi 25  na kwamba mawakala wa kununua
pareto vijijini watakuwa 15.
Alisema uwezo wa kiwanda hicho ni kusindika tani 750 kwa mwaka na kwa
kuanzia mwaka huu wanatarajia kusindika tani 300.
Hata hivyo aliiomba Serikali isaidie kupunguza changaoto za ubovu wa
barabara na ukosefu wa umeme ambapo hadi sasa wanatumia majenereta
kusindika mazao.
Akizungumza machache , Kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour
alipongeza ujenzi wa kiwanda hicho na kwamba unafanyika wakati
Serikali ya awamu ya Tano ikiwa kwenye harakati  ya kuhamasisha ujenzi
wa viwanda.





No comments