TUHUMA ZA WANAVIKUNDI KUTAPELIWA NA VICOBA, MAKALA ATOA AGIZO
Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, amemuagiza Ofisa maendeleo mkoani hapa kumwandikia barua rais wa Vicoba endelevu Tanzania Devotha Likokola, baada ya kulalamikiwa na wanakikundi cha Yuaja kwamba raisi huyo amekitapeli kikundi chao zaidi ya million mbili.
Makalla alifikia hatua jana kwenye kikao cha kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkapa jijini hapa, baada ya wanakikundi hao kulalamika kuwa wamefuatilia fedha hizo mara nyingi kwa Devotha lakini hatoa majibu ya kueleweka.
Alisema ‘’Nakuagiza Ofisa maendeleo kumwandikia barua huyo Devotha ili ajibu malalamiko haya yanayotolewa na wanakikundi na majibu yatakayotolewa kutoka kwake unipe niyaangalie halafu niangalia hatua za kuchukua,’’alisema Makalla
Awali Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Yuaja Christina Sendana, alisema rais huyo alifika mkoani hapa na kuwaeleza kuwa wampatie Sh1milioni ili wakopeshwe mara tatu na baadaye alidai kuwa waongeze Sh1 milioni ili waweze kukopesheka kirahisi .
‘’Kweli tuliongeza zile fedha na kufikia milioni mbili na zaidi lakini tulivyouliza mbona hiyo mikopo hatupewi alichojibu rais ni kwamba mratibu aliyekuwepo wakati ule alitoroka na fedha zetu na akaahidi kuwa ataleta mratibu mwingine wa kutusaidia ili tupate mkopo huo,’’alisema Sendana
Aliongeza ‘’Kweli alikuja mratibu mwingine kwa gharama zetu sisi wanakikundi na alikaa hapa siku tatu lakini naye baada ya kuangalia hundi ya benki alidai kuwa salio lililopo hatuwezi kukopesheka kwani hatuna fedha,’’alisema.
Sandana alibainisha kwamba hawakuridhika na majibu yaliyotolewa na mratibu huyo na kwamba walifunga safari kumfuata rais huyo kwa gharama zao lakini hakuweza kutoa majibu yanayoeleweka.
Naye Mkatibu wa Yuaja Halima Lyambo, alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2014 na kilikuwa na wanachama 15 ambao walikuwa wananunua hisa lakini kwa sasa wamebaki wachache baada ya kuona wamedhurumiwa fedha zao na raisi huyo.
‘’Malalamiko yetu tuliyafikisha kwa Ofisa Maendeleo ambaye alitusikiliza lakini na yeye akatuambia ni mzigo ambao hawezi kuubeba ndipo alitutuma kwa mkuu wa mkoa ili atusaidie jambo hili tulilofuatailia wa miaka mitatu sasa,’’alisema Halima.
Post a Comment