WAFANYA KAZI FEKI WASIFIKE MAY 15 JPM AAGIZA
Na Mwandishi wetu
Dodoma Rais Magufuli wa Tanzania amewafuta kazi wafanyikazi 10,000 wa serikali kwa kuwa na vyeti bandia vya elimu. Amewaagiza kuwacha kazi ifikiapo Mey 15 la sivyo wakamatwe na kushtakiwa.
Hatua hiyo inajiri baa wafanyikazi hao kupatikana na vyeti bandia vya shule.
Kulingana na ripoti iliopokewa na rais Magufuli, takriban wafanyikazi 10,000 wa serikali wana vyeti ghushi vya shule.
Maelezo hayo yaliotolewa katika mji mkuu wa Dodoma yanaonyesha wafanyikazi 9,932 wa serikali walipatikana na vyeti bandia vya shule ya upili idadi hiyo ni asilimia 2 ya wafanyikazi wote wa serikali wapatao 435,000.
Post a Comment