WALEMAVU WAPEWA ELIMU YA MAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Mbeya. Katika harakati za kupunguza mambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini,Hosptari ya Rufaa Kanda ya Mbeya imendesha elimu ya tohara na mambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa walemavu wa kusikia wanaoishi mkoani hapa.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo juzi, mratibu wa tohara kwa
wanaume hosptali ya Rufaa Majuni Mtagwaba alisema wamefikia hatua ya kutoa elimu kwa walemavu hao baada ya
viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Mbeya kupeleka maombi
ya kupatiwa elimu hiyo.
Mtagwaba alisema baada ya
hosptali kupata maombi hayo ,waliona kuna haja ya kutoa elimu hiyo kwani
makundi ya walemavu yamekuwa hayapati elimu hiyo kutokana changamoto ya
mawasiliano, hivyo kupelekea walemavu kukumbwa na mambukizi magonjwa mara
kwa mara kama kisonono,kaswende, gonolea pamoja na ukimwi.
“Makundi ya walemavu hasaViziwi
wamekuwa kinara wa kufanya ngono zembe kutokana na kutokuwa na elimu ya kujikinga na mambukizi ya ukimwi na mwitikio
wa kufanyanyiwa tohara haupo kabisa,ndiyo maana wemekuwa wakiambukizwa mara kwa
mara”,alisema.
Alisema,tohara kwa wanaume
inapunguza mambukizi yanayotokana na ngono kwa asilimia 60,ndiyo maana tumekuwa
tukihamasisha wananchi kujitokeza kufanyiwa tohara.s
Katibu wa chama cha viziwi
Mkoa wa Mbeya Queen Majembe alisema mafunzo hayo ni mara ya kwanza kupata kwa
walemavu hao na yamekuja muda mwafaka kutokana na kipindi hiki mambukizi ya
virusi yameshika kasi katika maeneo mbalimbali nchini.
Queen alisema,Mkoa wa
Mbeya una viziwi 7,000 na wengi hawana elimu ya tohara pamoja na mambukizi ya
virusi vya ukimwi hivyo ni vema taasisi mbalimbali zijitokeze kuhamasisha elimu
hiyo ili kunusuru jamii ya walemavu.
“Tunaishukuru Hosptali ya
Rufaa kwa kutupatia elimu hii ambayo itatusaidia kwa kiasi kikubwa katika jamii
tunazotoka lakini pia tutaisambaza kwa walemavu ambao hawajafika hapa leo hasa waliopo
wilayani”,alisema.
Naye mlemavu Epafula Isaya
alisema,awali walikuwa wanashindwa kwenda vituo vya afya kufanyiwa tohara kwani hawajahi kupewa elimu
ya faida za kufanyiwa tohara na hasara zake.
Post a Comment