TANI 14 ZA BIDHAA ZENYE SUMU ZATEKETEZWA NA TFDA
Mbeya. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imeteketeza tani 14 za bidhaa zenye viambata vya sumu na zilizopigwa
marufuku kuingizwa nchini zenye thamani ya Sh 248 kwa mwaka 2015/16.
Meneja wa TFDA kanda, Rodney Alananga alisema jana wakati akizungumza na mwananchi ofisini kwake na kutaja mikoa ya Songwe na Mbeya ndio vinara wa uingizwaji wa bidhaa ,hususan vipodozi na madawa kutoka nchi za jirani kupitia mipakani iliyopo.
Alisema kuwa bidhaa hizo zilikamatwa katika Mikoa ya Njombe, Iringa na Rukwa kwa kipindi cha mwaka 2015/16 katika msako uliohusisha mamlaka hiyo na jeshi la polisi na kwamba pia kuna wafanyabiashara waliosalimisha bidhaa hizo wenyewe kwenye mamlaka hiyo.
"Mbali na kuteketeza bidhaa hizo , kuna mashauri 40 ya wafanyabishara waliopatikana na bidhaa hizo na sasa mahakama mbalimbali mkoani hapa na kesi nyingi zinatarajia kuisha mwaka huu na mahakama ndiyo watakaoamua sheria za kuwachukulia ikiwemo ya kutozwa faini"alisema Alananga.
Alisema kuwa kati ya tani hizo 14,tani sita zilisalimishwa na wafanyabiashara wenyewe kabla ya mamlaka kuingia mitaani kufanya ukaguzi kwenye maduka ya vipodozi,vyakula na madawa .
''TFDA inajitahidi kutoa elimu kwa wafanyabishara na watumiaji wa bidha hizo lakini pia wafanyabishara wenyewe watii sheria kwa hiari
Mfanyabishara wa Vipodozi jijini hapa, Jastine Mwakikambako, alisema kuwa elimu inatolewe kwa wafanyabishara hususani kuimarisha ulinzi katika mipaka yetu ambayo ndio sehemu ya kuingiza bidhaa hizo kutoka nchi za jirani.
Naye mkazi wa mtaa wa ghana jijini hapa, Jane Saimon , alisema kuwa hata jamii inalojukumu la kusaidiana na Serikali katika vita ya kupiga marufuku bidhaa zenye viambata vya sumu vilizopigwa marufuku kuingizwa nchi.
"Tumeona wanawake wengi hususani hapa kwetu wanaharibika nyuso zao kutokana na kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa hiyo kwa suala hili si mtumiaji au muuzaji wote tunao wajibu wa kupiga vita suala hili,''alisema .
Post a Comment