Header Ads

WADAU WA ELIMU MBEYA WALIA NA MATOKEO MABAYA

Mbeya. Wadau wa elimu  na Viongozi wa dini ,  wameeleza mambo matatu yanayoweza kuongeza kiwango cha elimu  mkoani hapa , kuwa ni kuboreshamaslai ya walimu, kufundisha stadi za kilimo  mashuleni ili kuwepo nachakula cha kutosha na wanafunzi wapate mlo mmoja au  miwili kwa siku.

Wakizungumza na mtandao huu  kwa nyakati tofauti jana walisema  kuwalicha kufanyika Kongamano ya kujadili masuala ya elimu ,  kufuatiakuwepo kwa matokeo mabaya ya elimu ya msingi  kwa mwaka 2015/16 wameishauri Serikali kupitia Wizara husika  kuweka mipango mikakati itakayosaidia walimu kufanya kazi kwa wito na wanafunzi kusoma kwa kujituma.
Mhazini Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya, Zumba Yuleni, alisema kuwa tatizo la njaa mashuleni ni changamoto inayosababishawanafunzi kutokuwa na uelewa mzuri wa masomo na kuwa mizigo kwa walimu.
"Katika mkoa wetu kuna uwezekano mkubwa wazazi  wakawa ndio changamoto, katika  hilo Serikali ianzishe mtaala wa kufundika kilimo mashuleni kupitia kwa wataalam wake  ili shule ziweze kuwa na chakula na wanafunzi wapate walau mlo mmoja  hata miwili kwa siku"alisema.
Alisema kuwa Sekta ya elimu imekuwa na mzigo mkubwa wa kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi na Sekondari lakini changamoto kubwa ni kwa wazazi kutokuwa karibu na walimu na hivyo kuwakatisha tamaa katika kufundisha.
Askofu wa Kanisa la  la Evanjelical Brother hoof Tanzania, na Katibuwa viongozi wa Dini Mkoani hapa, Robby Mwakanani, alisema  endapo Serikali ikaweka mikakati ya kuboresha mazingira mazuri ya utendaji wa kazi na maslai ya  walimu,kuna uwezekano mkubwa mkoa wetu ukapiga hatua .

"Walimu wanaishi mazingira magumu sana hususan wa vijijini, hali inayowalazimu kuingia kwenye mikopo na mwisho wa siku mshahara wote unaishia kwenye madeni lakini kama Serikali ikasikiliza kilio chao kuna uwezekano  mkubwa kiwango cha elimu kikaongezeka kwa kiasi kikubwa"alisema.
April 5 Mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, aliitishaKongamano la kujadili masuala ya elimu kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali  , Viongozi wa Serikali  na lengo kuu lilikua kuona namna ya kuongeza kiwango cha ufauru kutokana na mkoa kuwa na matokeo mabaya kwa  2015/16.
Makalla, alisema kuwa baada ya Serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bure kwa mwaka 2017  jamii ilihamasika ambapo asilimia 115  ya watoto waliandikishwa elimu ya awali,  na darasa la kwanza asilimia104 .
"Ni jambo la kusikitisha kwa mwaka 2015 matokeo ya  elimu ya msingi lengo kitaifa  yalikuwa asilimia  75 kimkoa 57 lakini mkoa ulishikanafasi  21 wakati mwaka 2016 lengo kitaifa asilimia 80 kimkoa 60 mkoa wetu ulikuwa wa 22 kwa kweli hii ni aibu tupu tunahitaji kuwekamikakati kikamilifu"alisema.
Ofisa elimu Mkoa, Benedicto Sandi, alisema kuwa changamoto hiyoinatokana na usimamizi usio rasmi  kwa wazazi na walezi na kwambawakuu wa shule wanapaswa kuanzisha majukwaa ya kukutana na wazazikufanya maazimio ya kuinua kiwango cha elimu.


Aidha alisema kutokana na changamoto hiyo,  wameweka mikakati kutumia Sera ya elimu ya mwaka 2014 ya kuanza kuandikisha watoto walina umri wa miaka mitatu kuanza elimu.

No comments