BUSOKELO WAJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA
Mbeya.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Busokelo mkoani hapa Eston Ngilangwa
amewagiza watendaji wa kata na vijiji kusimamia na kuhakikisha wakulima wa zao
la ndizi hawauzi kiholela na badala yake wapeleke kwenye soko lililo jengwa
hivi karibuni.
Akizungumzia
hatua jana jijini hapa Ngilangwa alisema halmashauri ifikia hatua kujenga soko
la ndizi katika kata ya Lupata kutokana na hujuma za wafanyabiashara kwa
wakulima wa zao hilo.
“Kutokana na
ujenzi wa soko hili nimeagiza watenadaji wangu wawe ndiyo wasimamizi wa
kuhakikisha mkulima anapeleka ndizi zake
soko la Lupata na hukuna mkulima atakaeruhusiwa kuuza ndizi mashambani kama
ambavyo walizoea hapo awali hivyo wanatakiwa wapeleke sehemu ambapo serikali
tumepanga”alisema.
Ngilangwa
alisema kwanzishwa kwa soko hilo halmashauri itaweza kuwathibiti
wafanyabiashara ambao walikuwa wanakwepa kulipa ushuru na kuwarubuni wankulima
kwa bei za ajabu.
Makamu
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Lupata Uswege
Mbamba alisema ujenzi wa soko hilo utasaidia wakulima kunufaika kilimo chao kwani
serikali itaweka bei elekezi ambapo mkungu mmoja utauzwa sh12,000 kutoka 6,000
ya awali.
“Lengo la
halmashauri kujenga soko hili ni kutaka wakulima wanufaike na kilimo cha zao la
ndizi kwani wakulima walikuwa wanauza bei ambazo zilikuwa
hawazinufaishi”alisema.
Mbamba
aliongeza kuwa licha ya kujenga soko hilo lakini wananchi watahamasishwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili wakati
wote ziwe zinapatikana sokoni hapo,ikiwa ni sambamba na kuwaelimisha faida za
uwepo wa soko hilo.
Akiongea
hivi karibuni mkulima wa zao hilo kutoka kijiji cha Lusungo Bernad Mwansepe
alisema ujenzi wa soko hilo utaleta ukombozi kwa mkulima mmoja mmoja kutokana
na madarali kuthibitiwa.
“Tunaipongeza
halmashuri yetu kwa hatua waliyofikia ya kutaka wakilima kwanza kunufaika na
zao tunalo lima,na sisi kama wakulima tutongeza juhudi ya uzalishaji wa ndizi
kwa wingi kwani ukombozi umefika”alisema.
Mwansepe
aliongeza kuwa Serikali waongeze maofisa organi katika vijiji kwa ajili ya
kuwapa elimu ya kilimo cha kisasa wazalishaji,kwani ni kwa mda mrefu wamekuwa
wakiendesha shughuli za kilimo bila kupata ushauri kutoka kwa watalamu.
Post a Comment