Header Ads

KABAKA AFANYA ZIARA MBEYA


 KABAKA AFANYA ZIARA MBEYA

Mbeya. Chama Cha Mapinduzi  kinatarajia kutoa semina elekezi kwa viongozi wake katika ngazi za kata Wilaya na Mkoa,  ili kuepusha mliangiliano wa utendaji kazi ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara na kupelekea migogoro ya mara kwa mara.
Akizungumza na Jumuiya na wanawake jana  mkoani hapa, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo nchini Gaudentia Kabaka, alisema baada ya kuona kuna mgongano wa kuingiliana majukumu kati ya Wenyeviti pamoja na makatibu kitu ambacho kinapelekea utendaji kazi kukwama.
“Tunawatoa semina elekezi kwa wenyeviti,makatibu na wajumbe wa mabaraza kwanzia ngazi ya Kata,Wilaya na Mkoa mada zitakazo wasilishwa ni Rushwa,malezi,uongozi bora pamoja na ujasiliamali”,alisema.
Gaudentia alisema wataalamu wa kutoa mafunzo hayo tayali wameandaliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.
“Haya mafunzo ni ya nchi nzima lakini tunaenda Kanda kwa kanda ndiyo maana mwezi huu tutanzia Nyanda za Juu Kusini na badae kuhamia sehemu nyingine”,.
Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Mbeya Jacob Mwakasole, alisema “Wananchi pamoja na wanachama wa Ccm wanatamani kuona Ujio wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Magufuli kuja kuwasikiliza kero wanazokumbana nazo kwani tangu amechaguliwa hajafika kuongea na wananchi wake, tunaomba mama Kabaka mfikishie kilio cha wananchi wetu”.
Mwakasole alisema wananchi wa Mkoa wa Mbeya wamejawa na hamasa ya kumuona Rais baada kuridhika na utendaji kazi mzuri tangu aingie madakani.
Katibu wa Ccm Mkoa wa Mbeya Wilison Nkhambako alisema, Chama hicho kimeanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kutembelea miradi mbalimbali katika kila Wilaya na kugundua baadhi ya kasoro ambazo wataziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa ili zipatiwe ufumbuzi mapema.
Mwisho.

No comments