MADIWANI MBEYA DC WAPITISHA SH. 59 BILIONI BAJETI YA 2018/19
Mbeya. Baraza
la madiwani Halmashauri ya Mbeya mkoani hapa limepitisha bajeti ya Sh 59
bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali katika halmashauri hiyo.
Akiwasilisha bajeti hiyo jana
Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo Filbert Mbwilo ,alisema vipaumbele vikubwa
katika bajeti hiyo ni ujenzi wa Shule ya wasichana Garijembe pamoja na
Machinjio ya kisasa eneo la Utengule Usongwe.
Mbwilo alisema katika mwaka wa fedha ujao
Halmashauri imejipanga kusimamia, kukusanya mapato kutoka vyanzo vya ndani
pamoja na vyanzo vingine vitakavyofanya wafikie malengo ya bajeti hiyo.
Alisema katika bajeti hiyo ,vipaumbele
vikubwa ni kutengeneza machinjio ya kisasa itakayogharimu zaidi ya Sh 200
milioni huku vipaumbele vingine vikiwa ni kuboresha miundombinu ya elimu, afya
,elimu maji na vinginevyo.
“Lakini pia mwaka huu tumejipanga kudhibiti upotevu wa mapato katika kata zetu
tunatarajia kununua pikipiki kwa watendaji wa kata na vijiji ili iwe rahisi
kufikia maeneo ya vijijini kukusanya mapato na tozo mbalimbali zinazotoka kwa
wakulima na wafanyabishara, ‘’alisema.
Akichangia bajeti hiyo, Diwani wa kata ya Bonde la
Songwe ,Ayasi Ramadhani, alisema katika
mwaka wa fedha uliyopita kulikuwa changamoto ya ukusanyaji wa mapato kutokana
na mazao ya mahindi, viazi na pareto kukosa soko na kwamba halmashauri hiyo
inapata fedha zake kutoka katika mageti yanayovusha mazao hayo.
Diwani wa viti maalum Frola
Lucas,alisema ‘Katika mwaka wa fedha ujao naomba halmashuri yetu ibadilike
katika kukamirisha miradi ya awali ndipo tuanze upya kutokana na kwamba
tunamiradi mingi ambayo mpaka sasa kwa asilimia kubwa haijakamilika kutokana na
usimamizi mbovu”.
Alitoa mfano miradi zaidi ya
minne ya maji ambayo tangu mwaka 2013 hadi
sasa haiujakamilika na kwamba kutokamilika kwa miradi hyo kunachangia
kucheleweshwa utekelezaji wa miradi mipya kwa wananchi.
Kwa Upande wake mwenyekiti
wa Halmnashauri hiyo,Mwalingo Kisemba aliungana na madiwani hao kupitisha
bajeti hiyo na kumuomba Mkurugenzi kwa kushirikiana na kamati ya fedha
kuangaliua namna ya kukopa fedha kutoka taasisi yoyote ili waweze kununua gari
za kubeba taka katika halmashauri hiyo.
‘’Ni aibu kuona halmashuri
nzima hatuna gari hata moja kwa ajili ya kubeba taka na ndiyo maana magonjwa ya
mlipuko yanatukumba mara kwa mara kutokana na hili hebu mwaka huu mpya wa
bajeti tuje kivingine,’’alisema Kisemba.
Mwisho.
Post a Comment