Wazee 9,679 Mkoa wa Mbeya wameandikishwa na kupewa kadi kwa ajili ya matibabu bure.
Mbeya. Wazee 9,679 Jijini hapa
wameandikishwa na kupewa kadi kwa ajili ya
matibabu bure katika vituo vya afya na zahanati zilizopo ndani ya jiji
kulingana na sera ya afya inavyo sema.
Akizungumza
na mwandishi wa gazeti hili Ofisa ustawi wa jamii jiji la Mbeya Eva John
alisema zoezi la uandikishaji wa wazee bado unaendelea katika mitaa mbalimbali
ili kuhakikisha kila mzee anapata kadi hiyo huduma za matibabu bure.
Eva alisema
changamoto kubwa ni baadhi ya wazee hao bado
hawajahamasika kujitokeza maeneo tuliotenga kuja kuandikisha ili kupata vitambulisho
ambavyo vinatakiwa vionyeshwe sehemu ambapo watapatiwa huduma za matibabu.
“Changamoto
kubwa tulio nayo hapa ni kwamba wazee walipo jijini hapa bado hawajahamasika kuja
kwenye vituo vilivyo tengwa na watendaji wa kata kujiandikisha hivyo inapelekea
baadhi yao kuto kupewa kadi hizo kwa ajili ya matibabu bure”,alisema.
Eva
aliongeza kuwa “Hata kama mzee hana kadi akienda kituo chochote atapatiwa
matibabu bure kulingana na umri alionao ili mradi tu awe anaishi ndani ya jiji”,alisema.
Mkazi wa
majengo jijini hapa Ambangile Mwambusye,alisema kwa sasa dirisha la wazee kwa
ajili ya matibabu bure limekuwa likifanya huduma nzuri tofauti na awali.
“Tunaipongeza
serikali kwa kusimamia hudumu ya
matibabu bure kwa wazee kwa kweli huduma zimeboreshwa kwa hali ya juu sasa hivi
nimetoka kituo cha afya Kiwanja mpaka wamenihudumia vizuri na nimepewa
kipaumbele cha kuhudumiwa”,alisema.
Naye Brown
Ambindwile mkazi wa kata ya Ghana alisema licha kupewa kadi kwa ajili ya
matibabu bure lakini tatizo la uhaba dawa katika vituo vya afya na zahanati tunavyo
hudumiwa ni changamoto kubwa.
“Tunaomba
serikali kuongeza dawa katika vituo vya afya na zahanati kwani kuna mda
tunakosa kabisa hapa tunaambiwa tukanunue wakati huo sisi pesa hatuna hivyo
inatuwia vigumu sana kutafuta pesa ya kununulia madawa ambayo tunandikiwa na
watalam wetu”,alisema.
Post a Comment