Header Ads

MILIONI 39 KUKARABATI PAMPU ZA MAJI CHUNYA



Na Ezekiel Kamanga

Chunya Mbeya .Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imetoa shilingi milioni thelathini na
tisa kwa ajili ya ukarabati wa pampu za maji katika Kata mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya
Bosco Mwanginde alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo katika Baraza la
Madiwani liliofanyika katika ukumbi wa Sapanjo mwishoni mwa wiki.


Akisoma taarifa ya Mkuu wa Wilaya kwa niaba yake Afisa Tarafa ya
Kiwanja Shila Sheyo amesema hali ya usalama Kiwilaya ni nzuri ingawa
amesema kuwa kuna baadhi ya wahalifu wameanza kufanya maficho katika
maeneo ya wafugaji, machimbo na nyumba za Ibada. Amewataka madiwani
kutoa elimu kwa wananchi ili kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama
ili kuifanya Chunya kuwa salama na si ficho la wahalifu. 
Aidha Mkuu wa
Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amepiga marufuku wakulima kuuza mazao
yakiwa shambani na amewataka wafanyabiashara kupata vibali vya kununua
mazao kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya. Hivi
karibuni kumeibuka wafanyabiashara wanaotoka mikoa jirani na
kuwarubuni wakulima kwa kununua mahindi kwa gharama ya shilingi elfu
saba kwa debe hivyo Wilaya hiyo kuwa katika tishio la kukumbwa na baa
la njaa.

No comments