Header Ads

RAMBI RAMBI ZA YANGA ZA ZUA MASUMBWI MBEYA



Mbeya. Jinamizi limevamia Klabu ya Yanga Taifa hadi huku mikoani baada ya juzi jioni kutokea varangati la viongozi wa wanachama mkoani hapa  kupigana ngumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kila mmoja kujipangia majukumu yake bila kushirikisha viongozi wenzake.
Hii inatokea ikiwa ni siku kadhaa tu tangu uongozi wa  mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kufungua akaunti kwa ajili ya wanachama kuichangia klabu hiyo inayokubwa na ukata wa kifedha na habari mbaya zaidi ni wanachama hao sasa kugfikia hatua ya kuingia kwenye misubwi ya wazi.

Ugomvi huo ulitokana na Katibu msaidizi wa matawi Rajabu Mrisho kuitisha kikao na wanachama wenzake bila kumtaarifu Mwenyekiti wa wanachama hao mkoani hapa Lusajo Kifamba.
Rajabu aliliambia gazeti hili kwamba baraka  za kuitisha kikao hicho alipewa na katibu mkuu ,ambacho kilikuwa na lengo la kupeana semina namna ya kuhamasisha wanachama kuichangia timu.
"Tulikutana hapa ukumbi wa Tumaini ambapo lengo la kufanya mkutano huo ilikuwa ni  kupeana semina namna ya kuhamasisha wanachama waweze kuichangia timu yetu,na taarifa za kikao mwenyekiti alikuwa nazo ndiyo maana nilimtumia makamu wake ili ampe taarifa sababu Mimi na yeye hatuelewani vyema ".alisema Rajabu
"Sekunde chache tu baada ta kuanaza kwa kikao mwenyekiti aliingia na wajumbe wawili na kuanza kuuliza nani aliyeitisha kikao hicho ambacho yeye hakitambui na baada ya kusema hivyo akaanzisha vurugu kwa kunirushia ngumi na kuvunja viti,lakini bahati nzuri wajumbe wakatuliza ugomvi huo ambao kwa kweli ingefikia hatua tungeumizana kwa vitu ambavyo si vya msingi".
Naye Mwenyekiti wa wanachama hao mkoa Kifamba  alipoulizwa kuhus jambo hilo,alikana kufanya vurugu hizo na kwamba yeye alikwenda eneo hilo kwa lengo la kutaka uhalali wa kikao hicho ambacho alisisitiza kuwa hakuwa na taarifa yoyote.
‘’Hizo taarifa ni za uwongo kwani mimi sijamrushia katibu ngumi ila nilienda tu bada ya kusikia kwa baadhi ya watu wakinihoji kuwa kuna kikao kinafanyika kwa nini mimi sijaenda?,’’alihoji Kifamba.
Baadhi ya mashuhudi waliloshuhudia tukio hilo walilithibitishia gazeti hili kwamba ni kweli Mwenyekiti alivyoingia alimrushia ngumi Rajabu.
‘’Ukweli Lusajo alifika akionekana ni mtu wa jazba na alivyoingia tu hakuhoji kitu ila hatua yake ya kwanza ilikuwa ni kumrushia Katibu ngumi ambaye aliokolewa na wasamalia wema baada ya kuona ugomvi ule unaweza kuleta picha mbaya kwa Yanga Mbeya,’’alisema mmoja wa shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Peter.
Kwa taarifa iliyotolewa na mmoja wa viongozi wa zamani wa wanachama hao ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alidokeza  kwamba tangu Klabu ya Yanga ipoteze mechi dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa kwenye Uwanja wa  ya Sokoine jijini hapa,uongozi wa matawi mkoa wa Mbeya umekuwa ukirushiana lawama kwa madai kuwa kuna baada ya viongozi waliihujumu timu  na ndiyo chanzo cha timu hiyo kula kichapo.

No comments