AMOSI MAKALA AZINDUA MRADI WA MAJI WENYE KIASI CHA MILION 397 MAKONGOROSI CHUNYA
Na Ezekiel Kamanga
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezindua mradi wa maji katika
kijiji cha Mkola Kata ya Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia tatu tisini na
saba. Akifungua mradi huo Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa Wilaya zote
mkoaani Mbeya kuwaondoa watu wote waliovamia vyanzo vya maji.Hata
hivyo Makalla amewataka wananchi wa Mkola kuutunza mradi huo na
kuhamisha uwanja wa mpira ili chanzo hicho kisiingiliane na shughuli
za kibinadamu. Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa mkuu wa Wilaya ya
Chunya Rehema Madusa amesema ujenzi wa Mradi huo umeanza mwaka 2009
kwa ushirikiano baina ya wananchi, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya na
Serikali Kuu.
Naye Mkurugenzi mtendaji Sophia Kumbuli amesema kuwa
Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na wananchi wa Mkola watatafuta
eneo la kuhamishia uwanja wa mpira Halmashauri itatoa tingatinga kwa
ajili ya kusawazisha. Mradi huo mpya utanufaisha zaidi ya wananchi
elfu na maji yake hapana magari . Kwa upande wao wananchi wameushukuru
serikali kwa kukamilisha mradi huo na kuahidi kuutunza ili kuondoa
changamoto iliyokuwa inawakabili.

Post a Comment