MKUU WA WILAYA MBEYA AMUWEKA MAHABUSU MWENYEKITI WA KIJIJI
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul John Ntinika ameamuru kuwekwa mahabusu
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsenga Fredy Salehe kwa kukaidi wito wake wa
kumtaka afike ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Alimwakilisha Mkuu wa Wilaya
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Hassan Mkwawa amesema mara kadhaa
Mwenyekiti huyo ameitwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kutokana na
malalamiko ya wananchi ya kufunga mfereji wa maji kinyume cha sheria.
Aidha Mkwawa amesema hivi karibuni amekataa kupokea mifuko kumi ya
saruji iliyotolewa na wahisani wa kikundi cha umwagiliaji wa HASHIMILA
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mganga . Katibu Tawala amesema
viongozi wa namna hiyo hatawafumbia macho kwa kuzorotesha maendeleo
ambapo Serikali inafanya juhudi ya kuhahakikisha kila kijiji kina
Zahanati. Licha ya kukataa saruji Mkwawa amesema kitendo cha kufunga
mfereji ni kosa kwani amesababisha hasara kwa wakulima kutokana na
kukauka mazao yao.
Baada ya kuwekwa mahabusu mkuu wa Wilaya amemwagiza
mtendaji wa kijiji kusimamia mfereji huo unafanyiwa usafiri na
wakulima wanaendelea na kilimo kama kawaida na kufanyika uchaguzi wa
kamati ya umwagiliaji.

Post a Comment