Header Ads

UVUVI HARAMU WASHAMIRI ZIWA RUKWA

Licha ya Serikali kulifunga ziwa Rukwa mara kwa mara na kupiga vita
uvuvi haramu lakini bado baadhi ya wavuvi wamekaidi amri hiyo na
kuendelea kuvua samaki kwa kutumia makokoro.Hali hiyo imesababisha
wavuvi hao kuharibu mazalia ya samaki na ziwa hilo kuwa hatarini
kupoteza viumbe hai katika ziwa hilo kwani hata samaki wanaaovuliwa
kwa sasa hawaafikii hata nchi mbili.

                                                                 
 Pamoja na kuwepo watumishi
waliopewa dhamana ya kusimamia ziwa hilo wakiwemo maafisa uvuvi na
watendaji lakini hawatimizi majukumu yao kutokana na kutokuwa na zana
bora kama maboti kwa ajili ya doria.
                                                                                                                                                                                                                     Aidha licha ya kutokuwa na zana
hizo rushwa inachangia kutokamatwa kwa wavuvi haramu, mbaya zaidi hata
walinzi waliopo katika mageti ya kukusanya ushuru hupokea tozo kwa
bidhaa haramu.Uchunguzi umebaini kuwepo kwa samaki kutoka ziwa Rukwa
walio chini ya nchi mbili huku makokoro yakiuzwa bila hiana Wilaya ya
Songwe, Momba na Mbozi bila kuchukuliwa hatua zozote.Eneo la Maleza
ndiyo imekuwa maficho makubwa ya wavuvi haramu katika Wilaya ya
Songwe.

No comments