SAKATA LA VYETI FEKI LA YUMBISHA UTENDAJI KAZI MBEYA
Mbeya.Halmashauri ya jiji la Mbeya inakabiliwa na changamoto ya kuyumba katika utendaji kazi katika kutoa huduma kwa jamii kutokana na watumishi 64 kukumbwa na sakata la vyeti feki huku awali ikiwa na upungufu wa watumishi 351 katika Idara tano zilizoathirika na zoezi hilo.
Hayo yalisemwa jana na ofisa habari wa halmashauri ya jiji la Mbeya John Kilua alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusiana na athari zizilizotokana na sakata la vyeti vya kugushi ambapo halmashauri hiyo watumishi 64 wameondolewa.
"Hali ni mbaya katika utoaji huduma kwa jamii kwa mfano maofisa watendaji kata sita wameondolewa ambapo utendaji wao upo jirani na Wananchi na hivyo imelazimu kuwatumia watendaji wa mitaa kufanya kazi mbili na ya kata"alisema
Alisema kuwa katika idara ya afya kuna wataalam ambao wamekuwa wakitoa huduma na kutegemewa katika zahanati na vituo vya afya wameondolewa na hivyo kusababisha kuyumba kwa utoaji huduma.
Naye ofisa utumishi wa halmashauri hiyo Gerald Ruzika alisema jumla ya watumishi 403 walihakikiwa ambapo 64 walikutwa na vyeti vya kugushi,14 vyeti vya utata na 110 vyeti vyao havijakamilika.
Alisema katika idadi hiyo ya 64 ya watumishi wenye vyeti vya kugushi,Elimu ya Msingi ni 23,Elimu ya Sekondari watumishi 4 upungufu uliokuwepo awali ilikuwa 153 na Idara ya Afya 24 upungufu wa awali ni 160.
Alizitaja idara nyingine kuwa ni Utawala ambapo watumishi walioondolewa ni 11 awali ilikuwa na upungufu wa watumishi 23,Ujenzi ni mmoja na awali upungufu ulikuwa wanne na idara ya mifugo mtumishi mmoja wakati awali upungufu ilikuwa 31.
Aidha alisema tayari wameshaandaa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na athari zinazotokana na changamoto ya kuondoa watumishi,ikiwa ni pamoja na kuomba kibali cha dharula cha ajira mbadala.
Mwisho

Post a Comment