MAMILIONI YA FEDHA MBARALI YALIVYOTUMIKA
Mbarali. Shilingi Milion 62 zimetumika kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana mwaka wa fedha 2016/17 katika Halmashuri ya Mbarali mkoa wa Mbeya .
Akitoa tarifa hiyo jana kwa wenyeviti wa mitaa katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rujewa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Kivuma Msangi alisema halmashauri katika mwaka wa fedha unaoisha mwezi Juni ilitenga Sh.80 kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana.
Msangi alisema katika Sh. 80 ni million Sh. 18 million zimekosa vikundi vya kukopesha kwa upande wa vijana kutokana na vikundi hivyo kukosa sifa ya kupewa mkopo.
“Katika Halmashauri yetu kuna vikundi 100 vya vijana lakini vimekosa sifa ya kupata mikopo kutokana na vikundi hivyo kuundwa kisiasa,mbali na siasa kuna vingine wajumbe wa vikundi wamezidi umri”alisema.
Aliongeza kuwa “Mbali na vikundi hivyo kukosa sifa lakini vijana wa wilaya ya Mbarali hawana hamasa kabisa ya kuunda vikundi hivyo natumaini wenyeviti wa mtaa mkitoka hapa mkafanye kazi ya kuhamasisha vijana kuunda vikundi bila kuangalia itikadi za vyama vyao ili waje wapate mikopo.”
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Rujewa Ayubu Chaula alisema vikundi vingi katika mji huo vimekuwa vikikosa sifa ya kupata mikopo kutokana kujikita kwenye kisiasa ziadi .
Chaula alisema kutokana na tarifa ya fedha kukosa vikundi vya kukopeshwa hivyo ni jukumu la kila mwenyekiti wa mtaa kuhamasisha vijana waunde vikundi ili wapate kujiajili wenyewe na Mamlaka Mji mdogo ikapata kodi kupitia biashara zao watakazo zianzisha.
“Mji wa Rujewa una vijana wengi ambao wanaweza kujiajili wenyewe kupitia mikopo hii inayotolewa na halmashauri lakini vijana wetu wa Rujewa wamejikita sana kwenye siasa kuliko kufanya maendeleo hivyo wenyeviti wa mitaa tujitahidi kufanya uhamasishaji wa vijana wetu kuunda vikundi na wajiajili”alisema.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mbuyuni Bobu Hamis alisema kwa kuwa wenyeviti wa mitaa ndiyo watambuzi wa vikundi hivyo,watahakikisha wanaitisha mikutano ya hadhara kwa ajili ya uhamasishaji.
“Hapa Rujewa tuna vijana wengi wenye nguvu na wasomi hivyo tukifanya uhamasishaji kupitia mikutano yetu ya hadhara vijana wetu watajitokeza wa wingi kuunda vikundi hivyo”,alisema.
MWISHO.

Post a Comment