Header Ads

MIMBA ZA UTOTONI KYELA TATIZO LA KITAIFA



Mbeya. Shirika la kiraia la Jitambue Lembuka Tanzania (JLT) mkoani hapa limeanza kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule zote namna ya kuepuka  na kijikinga  mimba za utotoni Katika Wilaya ya Kyela.

Akizungumza na mwandishi wetu juzi wilayani humo mkurugenzi wa shirika hilo Simon Mkanya alisema elimu hiyo itatolewa kwa shule za msingi na Sekondari kwa kuwashilikisha wadau wa elimu wilayani humo.

Mkanya alisema wameamua kutoa elimu hiyo kutokana na tatizo hilo kuwa sugu katika Wilaya Kyela kitu ambacho kimepelekea kuporomoka kwa elimu katika shule zilizopo wilayani humo.


“Elimu hii ambayo tunaitoa huwa tunawashirikisha wazazi na walezi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu, ili wote watambue njia za namna ya kukumbana mimba za utotoni”alisema Mkanya.

Takwimu za mimba za utotoni katika wilaya ya Kyela zinaonyesha kuwa kwanzia mwaka 2010 mpaka sasa ni Zaidi ya wanafunzi 645 wakitisha masomo kutokana na mimba za utotoni.

Afisa maendeleo ya Jamii wilayani humo Omary Mungi alisema kutokna na takwimu hizo kuna umuhimu  halmashauri kuunga mkono juhudi za shirika hilo ili kutokomeza mimba za utotoni na kudumisha elimu.

“Naishukuru Lembuka kwa kutambua  hili baada ya miezi miwili litaleta matokeo chanya katika wilaya yetu hivyo na mimi  ntahakikisha nalifikisha kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ili aliangalie namna ya kuunga mkono juhudi hizi”alisema.

Mkazi wa kijiji cha Nkuyu Wilayani humo Sophia Mwansampeta alisema baadhi ya wazazi wamekuwa ni tatizo pindi watoto wao wanapopewa ujauzito wanakuwa wakipokea mahali (pesa au ng’ombe) na kushindwa kutoa ushirikiano mahakamani.

“kwa kipindi hiki sasa ni jukumu latu wazazi kushilikiana na serikali katika kutokomeza mimba za utotoni kutokana watoto wengi wanashindwa kutimiza ndoto zao”alisema.

No comments