Header Ads

BAYPORT KUPAMBANA NA VYOO VIBOVU BUSOKELO




 Kampuni ya Bayport inanyojishugulisha na utoaji mikopo kwa watumishi mkoani hapa imetoa misaada ya mifuko ya saruji 30 kwa Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe kwa ajili ya kutatua changamoto upungufu wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Lwangwa.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi saruji hizo meneja wa Baypot Nyanda za Juu Kusini Mohamed Kissoki alisema wameamua kutoa misaada ilikuunga mkono juhudi za serikali za kutaka kuboresha elimu nchini hasa katika miundombinu.

Kissoki alisema mpango huo hautokomea katika halmashuri ya Busokelo bali ni mpango endelevu katika  Wilaya zingine ili kuhakisha watoto wanaepukana adha wanazokumbana nazo wakiwa mashuleni.


“Sisi kama kampuni tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ili kuhakikisha watoto wetu wanasomea mazingira safi”alisema.





Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Eston Ngilangwa alisema msaada huo umekuja wakati mwafaka kutokana na halmashauri hiyo kuwa na upungufu wa matundu ya vyoo 1200 kwa shule za msingi na matundu 85 kwa shule za sekondari.

“Naipongeza sana hii kampuni ya Baypot kwa msaada iliyotoa katika halmashauri yetu kwani sasa hivi tuna mpango mkakati wa kuhakikisha kufika oktoba mwaka huu changamoto hii  iwe imetatuliwe”alisema.

Meneja masoko wa Baypot mkoa wa Mbeya Samwel Ayubu alisema kampuni hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika halmashauri kutokana na kwamba watumishi ndiyo wateja wao kwa asilimia kubwa.

“Huu msaada tulio utoa leo wa mifuko ya saruji 30 umegharimu Sh. 300,000 na hatutaishia kutoa mifuko ya saruji tu kwani sasa hivi tuna mpango wa kutoa komputa tatu kila halmashauri za mkoa wa Mbeya na Songwe”alisema.

No comments